Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 9:15 - Swahili Revised Union Version

15 Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hasori, na Megido, na Gezeri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Yafuatayo ni maelezo juu ya jinsi mfalme Solomoni alivyotumia kazi za kulazimishwa kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu, ikulu yake, ngome ya Milo na ukuta wa Yerusalemu, na pia katika kujenga upya miji ya Hazori, Megido na Gezeri;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Yafuatayo ni maelezo juu ya jinsi mfalme Solomoni alivyotumia kazi za kulazimishwa kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu, ikulu yake, ngome ya Milo na ukuta wa Yerusalemu, na pia katika kujenga upya miji ya Hazori, Megido na Gezeri;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Yafuatayo ni maelezo juu ya jinsi mfalme Solomoni alivyotumia kazi za kulazimishwa kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu, ikulu yake, ngome ya Milo na ukuta wa Yerusalemu, na pia katika kujenga upya miji ya Hazori, Megido na Gezeri;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Haya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Sulemani aliwafanyiza watu ili kulijenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, na jumba lake la kifalme, na Milo, ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Haya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Sulemani, alivyowafanyiza watu ili kulijenga hekalu la bwana, na jumba lake la kifalme, na Milo, ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 9:15
34 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani.


Na hii ndiyo sababu ya yeye kumwasi mfalme. Sulemani aliijenga Milo, akapafunga palipobomoka pa mji wa baba yake Daudi.


Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa utupunguzie utumwa mzito tuliotumikishwa na baba yako, na lile kongwa zito alilotutwika, nasi tutakutumikia.


Huyo Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi, hata alipokwisha kuijenga nyumba yake, na nyumba ya BWANA, na ukuta wa kuuzunguka Yerusalemu.


Baana mwana wa Ahiludi, katika Taanaki na Megido, na Beth-sheani yote, iliyo kando ya Sarethani, chini ya Yezreeli, tangu Beth-sheani mpaka Abel-mehola, hata kupita Yokmeamu.


Mfalme Sulemani akakusanya kutoka kila mahali katika Israeli watu wa shokoa nao walikuwa elfu thelathini.


Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.


Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alizijenga zile nyumba mbili, nyumba ya BWANA na nyumba yake mfalme,


watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.


Lakini binti Farao akapanda toka mji wa Daudi, mpaka hiyo nyumba yake Sulemani, aliyomjengea; kisha, aliijenga Milo.


Nao watumishi wake wakaondoka, wakala njama, wakamwua Yoashi katika nyumba ya Milo, hapo panaposhukia Sila.


Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.


Na Ahazia mfalme wa Yuda alipoona hayo, akakimbia kwa njia ya nyumba ya bustanini. Yehu akamfuatia, akasema, Mpigeni huyu naye katika gari lake; wakampiga hapo penye kupandia Guri, karibu na Ibleamu. Akakimbilia Megido, akafa huko.


Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai; nao Wafilisti wakashindwa.


Basi wakapewa miji ya kukimbilia, yaani, Shekemu pamoja na viunga vyake katika nchi ya milima milima ya Efraimu; na Gezeri pamoja na viunga vyake;


Lakini Yosia hakukubali kumwachia, akajibadilisha apate kupigana naye, asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani kwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido.


Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani aliijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe;


Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako, Uzijenge kuta za Yerusalemu.


Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.


Wakati huo Horamu, mfalme wa Gezeri, akakwea ili kuusaidia Lakishi, lakini Yoshua akampiga yeye na watu wake, hata asimsazie hata mtu mmoja.


Kisha ikawa, hapo huyo Yabini, mfalme wa Hazori, aliposikia habari ya mambo hayo, akatuma mjumbe aende kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na mfalme wa Akshafu,


Nao hawakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa Gezeri; lakini hao Wakanaani waliketi kati ya Efraimu, hata hivi leo, wakawa watumishi wa kufanya kazi za shokoa.


kisha ikateremkia upande wa magharibi hadi kuufikia mpaka wa Wayafleti, hadi mpaka wa Beth-horoni ya chini, hadi kufikia Gezeri; na matokeo yake yalikuwa hapo baharini.


Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Beth-sheani na vijiji vyake, Ibleamu na miji yake, wenyeji wa Dori na miji yake, wenyeji wa Endori na miji yake, wenyeji wa Taanaki na miji yake, wenyeji wa Megido na miji yake, na pia theluthi ya Nafathi.


Adama, Rama Hazori;


Nao wakawapa Shekemu pamoja na mbuga zake za malisho, katika nchi ya vilima ya Efraimu, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Gezeri pamoja na mbuga zake za malisho;


Efraimu naye hakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa katika Gezeri; lakini Wakanaani walikaa ndani ya Gezeri kati yao.


BWANA akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa kamanda wa jeshi lake.


Wafalme walikuja wakafanya vita, Ndipo wafalme wa Kanaani walifanya vita. Katika Taanaki, karibu na maji ya Megido; Hawakupata faida yoyote ya fedha.


lakini ikiwa basi moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki.


Kisha hao watu wote wa Shekemu wakakusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na kumtawaza Abimeleki awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo katika Shekemu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo