Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 8:1 - Swahili Revised Union Version

1 Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa makabila na wakuu wa koo za wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la Agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Basi, mfalme Solomoni akawakutanisha mbele yake huko Yerusalemu wazee na viongozi wote wa makabila na wa koo za Israeli ili waliondoe sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu katika mji wa Daudi, yaani Siyoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Basi, mfalme Solomoni akawakutanisha mbele yake huko Yerusalemu wazee na viongozi wote wa makabila na wa koo za Israeli ili waliondoe sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu katika mji wa Daudi, yaani Siyoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Basi, mfalme Solomoni akawakutanisha mbele yake huko Yerusalemu wazee na viongozi wote wa makabila na wa koo za Israeli ili waliondoe sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu katika mji wa Daudi, yaani Siyoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kisha Mfalme Sulemani akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kisha Mfalme Sulemani akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa makabila na wakuu wa koo za wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la Agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 8:1
25 Marejeleo ya Msalaba  

Hata walipofika kwenye uga wa Nakoni, Uza akalinyoshea mkono sanduku la Mungu, akalikamata kwa maana wale ng'ombe walijikwaa.


Basi Daudi akalala na babaze, akazikwa mjini mwa Daudi.


Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la Agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.


Basi Daudi akakaa ngomeni; kwa hiyo ukaitwa mji wa Daudi.


Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na makamanda wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la Agano la BWANA kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;


Hata ikawa, sanduku la Agano la BWANA lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake.


Basi Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu, ili kulipandisha sanduku la BWANA, mpaka mahali pake alipoliwekea tayari.


Kisha Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa kabila, na makamanda wa vikosi wenye kumtumikia mfalme kwa zamu, na makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, na wenye kutawala juu ya mali na milki za mfalme, na za wanawe, pamoja na matowashi, na mashujaa, naam, wanaume mashujaa wote.


Hezekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda pia; akawaandikia nyaraka Efraimu na Manase, waje nyumbani kwa BWANA Yerusalemu, ili wamfanyie Pasaka BWANA, Mungu wa Israeli.


Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu.


Watu walitangaze jina la BWANA katika Sayuni, Na sifa zake katika Yerusalemu,


Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni, Yatangazeni kwa watu matendo yake.


kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.


Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.


Tena mwanamume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi; kila mmoja aliye kichwa cha nyumba ya baba zake.


Yoshua akawaita Israeli wote, wazee wao, na wakuu wao, na waamuzi wao, na makamanda wao, akawaambia, Mimi ni mzee, nami nimezeeka sana;


Yoshua akawakusanya makabila yote ya Israeli huko Shekemu, akawaita wazee wa Israeli, na wakuu wao, na waamuzi wao, na maofisa wao nao wakaja mbele za Mungu.


Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo