Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Wafalme 7:16 - Swahili Revised Union Version

16 Akatengeneza mataji mawili ya shaba iliyoyeyushwa ya kuwekwa juu ya vichwa vya nguzo; kwenda juu kwake taji moja mikono mitano, na mikono mitano kwenda juu kwake taji la pili.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Akatengeneza pia taji mbili za shaba, kila moja ikiwa na kimo cha mita 2.25; akaziweka juu ya nguzo hizo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Akatengeneza pia taji mbili za shaba, kila moja ikiwa na kimo cha mita 2.25; akaziweka juu ya nguzo hizo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Akatengeneza pia taji mbili za shaba, kila moja ikiwa na kimo cha mita 2.25; akaziweka juu ya nguzo hizo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Pia alitengeneza mataji mawili ya shaba ya kusubu ili kuyaweka juu ya hizo nguzo; kila taji lilikuwa na kimo cha dhiraa tano kwenda juu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Pia alitengeneza mataji mawili ya shaba ya kusubu ili kuyaweka juu ya hizo nguzo; kila taji lilikuwa na kimo cha dhiraa tano kwenda juu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Akatengeneza mataji mawili ya shaba iliyoyeyushwa ya kuwekwa juu ya vichwa vya nguzo; kwenda juu kwake taji moja mikono mitano, na mikono mitano kwenda juu kwake taji la pili.

Tazama sura Nakili

1 Wafalme 7:16
8 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana alizifanyiza zile nguzo mbili za shaba, mikono kumi na minane kwenda juu kwake kila moja; na uzi wa mikono kumi na miwili kuizunguka nguzo hii au hii.

Kulikuwa na nyavu kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa mataji yaliyokuwako juu ya vichwa vya nguzo; saba kwa taji moja, na saba kwa taji la pili.

na nguzo zake tano pamoja na kulabu zake; naye akavifunika dhahabu vichwa vyake na vifungo vyake; na vitako vyake vitano vilikuwa ya shaba.

Na vitako vya zile nguzo vilikuwa vya shaba; kulabu za hizo nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha; na vichwa vya zile nguzo vilikuwa ni vya fedha; na nguzo zote za huo ua ziliungwa kwa vitanzi vya fedha.

Na nguzo zake zilikuwa nne, na vitako vyake vinne, vilikuwa vya shaba; kulabu zake zilikuwa za fedha, na vichwa vyake na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha.

Na kwa hizo shekeli elfu moja na mia saba, na sabini na tano, akafanya vifungo vya hizo nguzo, na kuvifunika fedha vile vichwa vyake, na kufanya vitanzi vyake.

Nayo ilikuwa na kichwa cha shaba juu yake; na urefu wa kichwa kimoja ulikuwa dhiraa tano; palikuwa na mapambo ya wavu na makomamanga juu ya kichwa hicho pande zote; vyote vilikuwa vya shaba; nayo nguzo ya pili ilikuwa na mapambo kama hayo, na makomamanga.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo