Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 4:28 - Swahili Revised Union Version

28 Shayiri pia na majani kwa farasi, na kwa wanyama wenye mbio, wakaleta mahali walipokuwapo, kila mtu kwa kadiri ya kazi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Zamu ya kila mmoja ilipofika, alipeleka pia shayiri na majani ya kulisha farasi na wanyama waendao kasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Zamu ya kila mmoja ilipofika, alipeleka pia shayiri na majani ya kulisha farasi na wanyama waendao kasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Zamu ya kila mmoja ilipofika, alipeleka pia shayiri na majani ya kulisha farasi na wanyama waendao kasi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Pia walileta kiasi walichopangiwa cha shayiri na majani kwa ajili ya farasi wa magari ya vita na farasi wengine mahali palipostahili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Pia walileta sehemu walizopangiwa za shayiri na majani kwa ajili ya farasi wavutao magari na farasi wengine mahali palipostahili.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 4:28
4 Marejeleo ya Msalaba  

Na maofisa wale wakaleta chakula kwa mfalme Sulemani na kwa wote walioijia meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake, kisipunguke kitu.


Akaandika kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutia mhuri kwa pete ya mfalme, barua zikapelekwa na matarishi, wamepanda farasi, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, ndio waliozalishwa katika zizi la mfalme.


Matarishi wakaondoka, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, huku wakihimizwa na kusukumizwa kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Susa mjini.


Mfungie gari la vita farasi Aliye mwepesi, wakazi wa Lakishi; Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni; Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo