Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 3:13 - Swahili Revised Union Version

13 Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Pia, nitakupa yale ambayo hukuomba: Nitakupa utajiri na heshima zaidi ya mfalme mwingine yeyote wa nyakati zako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Pia, nitakupa yale ambayo hukuomba: Nitakupa utajiri na heshima zaidi ya mfalme mwingine yeyote wa nyakati zako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Pia, nitakupa yale ambayo hukuomba: nitakupa utajiri na heshima zaidi ya mfalme mwingine yeyote wa nyakati zako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba: utajiri na heshima; siku za maisha yako yote hapatakuwa na mtu kama wewe miongoni mwa wafalme.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba, yaani utajiri na heshima, ili kwamba maisha yako yote hapatakuwa na mtu kama wewe miongoni mwa wafalme.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 3:13
14 Marejeleo ya Msalaba  

Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani mwaka mmoja, ndio talanta mia sita sitini na sita,


Naye BWANA akamtukuza Sulemani mno machoni pa Israeli wote, akampa fahari ya kifalme ya kumpita mfalme awaye yote aliyekuwa kabla yake katika Israeli.


Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima.


Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.


Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.


Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji la uzuri.


mtu aliyepewa na Mungu mali, ukwasi, na heshima, hata asipungukiwe na kitu chochote kwa nafsi yake, katika yote anayoyatamani lakini Mungu hamwezeshi kula katika hizo; bali mgeni hula. Hayo ndiyo ubatili hasa, nayo ni ugonjwa mbaya.


Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.


Yeye ambaye hakumhurumia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje pia kutupa chochote kingine pamoja naye?


Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo