Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 22:40 - Swahili Revised Union Version

40 Basi Ahabu akalala na baba zake; na Ahazia mwanawe akatawala mahali pake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Ahabu alipofariki, mwanawe Ahazia alitawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 Ahabu alipofariki, mwanawe Ahazia alitawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Ahabu alipofariki, mwanawe Ahazia alitawala mahali pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Ahabu akalala na baba zake. Naye Ahazia mwanawe akawa mfalme baada yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Ahabu akalala pamoja na baba zake. Naye Ahazia mwanawe akawa mfalme baada yake.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 22:40
13 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitauimarisha ufalme wake.


Naye Hadadi aliposikia huko Misri ya kuwa Daudi amelala na babaze, na Yoabu, jemadari wa jeshi, amekufa, Hadadi akamwambia Farao, Unipe ruhusa, niende mpaka nchi yangu.


Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala mahali pake.


Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na jina la mamaye aliitwa Naama, Mwamoni. Na mwanawe, Abiya, alitawala mahali pake.


Basi Daudi akalala na babaze, akazikwa mjini mwa Daudi.


Na mambo yote ya Ahabu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na nyumba ya pembe aliyoijenga, na miji yote aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?


Yehoshafati mwana wa Asa alianza kutawala juu ya Yuda, katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli.


Ahazia mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria, katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka miwili juu ya Israeli.


Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya babaye, na njia ya mamaye, na njia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli.


Basi akafa, sawasawa na neno la BWANA alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana.


Na Ahazia akaanguka kutoka dirisha la chumba chake ghorofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Nendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona ugonjwa huu.


Baada ya hayo Yehoshafati mfalme wa Yuda akapatana na Ahazia mfalme wa Israeli; naye huyo ndiye aliyefanya mabaya mno;


BWANA akamwambia Musa, Angalia, wewe utalala na baba zako; na watu hawa wataondoka, wataifuata kwa ukahaba miungu ya kigeni ya nchi waiendeayo kuwa kati yao, nao wataniacha mimi na kulivunja agano langu, nililofanya nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo