Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 20:15 - Swahili Revised Union Version

15 Ndipo akawakusanya vijana wa watawala wa majimbo, nao walikuwa mia mbili thelathini na wawili; kisha baada ya hao akawakusanya watu wote, wana wa Israeli wote, nao walikuwa elfu saba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Basi, mfalme Ahabu akakagua vijana waliotumikia jeshi chini ya wakuu wa wilaya, jumla yao watu 232. Kisha akakagua jeshi la Israeli, wanajeshi 7,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Basi, mfalme Ahabu akakagua vijana waliotumikia jeshi chini ya wakuu wa wilaya, jumla yao watu 232. Kisha akakagua jeshi la Israeli, wanajeshi 7,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Basi, mfalme Ahabu akakagua vijana waliotumikia jeshi chini ya wakuu wa wilaya, jumla yao watu 232. Kisha akakagua jeshi la Israeli, wanajeshi 7,000.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Hivyo, Ahabu akawaita maafisa vijana wapatao mia mbili thelathini na wawili (232) waliokuwa chini ya majemadari wa majimbo. Kisha akawakusanya Waisraeli waliobaki, ambao idadi yao walikuwa elfu saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kwa hiyo Ahabu akawaita maafisa vijana majemadari wa majimbo, wanaume 232. Kisha akawakusanya Waisraeli wote waliobaki, jumla yao 7,000.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Ndipo akawakusanya vijana wa watawala wa majimbo, nao walikuwa mia mbili thelathini na wawili; kisha baada ya hao akawakusanya watu wote, wana wa Israeli wote, nao walikuwa elfu saba.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 20:15
11 Marejeleo ya Msalaba  

Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.


Ahabu akanena, Kwa nani? Akasema, BWANA asema hivi, Kwa vijana wa watawala wa majimbo. Ndipo akanena, Ni nani atakayepanga vita? Naye akajibu, Ni wewe.


Wakatoka wakati wa adhuhuri. Lakini Ben-hadadi alikuwa akinywa hata kulewa mabandani, yeye na wale wafalme thelathini na wawili waliomsaidia.


Kwa kuwa hakumwachia Yehoahazi watu ila wapandao farasi hamsini, na magari kumi, na askari elfu kumi waendao kwa miguu; kwa kuwa mfalme wa Shamu aliwaharibu, akawaponda mfano wa mavumbi yaliyokanyagwa.


Naye Asa akamlilia BWANA, Mungu wake, akasema, BWANA, hapana kuliko wewe aliye wa kusaidia, kati yake yeye aliye hodari, na yeye asiye na nguvu; utusaidie, Ee BWANA, Mungu wetu; kwa kuwa sisi twakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja juu ya jamii kubwa hii. Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu wetu, asikushinde mwanadamu.


Mfalme haokolewi kwa jeshi lake kubwa, Wala shujaa haokoki kwa kuwa na nguvu nyingi.


Kisha akawapanga wale watu mia tatu wawe vikosi vitatu, akatia tarumbeta katika mikono ya watu wote, na mitungi isiyo na maji, na mienge ndani ya hiyo mitungi.


BWANA akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu mahali pake.


Naye Sauli alikuwa akikaa katika Viunga vya Gibea, chini ya mkomamanga uliokuwa kwenye uwanja huko Migroni; na hao watu waliokuwa pamoja naye walikuwa watu mia sita;


Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha zake, Haya! Na twende tukavuke ngomeni mwa hao wasiotahiriwa; yamkini BWANA atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia BWANA asiokoe, kama ni kwa wengi au kama ni kwa wachache.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo