Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Wafalme 2:27 - Swahili Revised Union Version

27 Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa BWANA; ili alitimize neno la BWANA, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Basi, mfalme Solomoni akamfukuza Abiathari, asiwe kuhani wa Mwenyezi-Mungu; hivyo likatimia neno alilosema Mwenyezi-Mungu huko Shilo, juu ya Eli na ukoo wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Basi, mfalme Solomoni akamfukuza Abiathari, asiwe kuhani wa Mwenyezi-Mungu; hivyo likatimia neno alilosema Mwenyezi-Mungu huko Shilo, juu ya Eli na ukoo wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Basi, mfalme Solomoni akamfukuza Abiathari, asiwe kuhani wa Mwenyezi-Mungu; hivyo likatimia neno alilosema Mwenyezi-Mungu huko Shilo, juu ya Eli na ukoo wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Hivyo Sulemani akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa Mwenyezi Mungu, akilitimiza neno la Mwenyezi Mungu alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Hivyo Sulemani akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa bwana, akilitimiza neno la bwana alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

27 Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa BWANA; ili alitimize neno la BWANA, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo.

Tazama sura Nakili

1 Wafalme 2:27
13 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, mahali pake juu ya jeshi; na Sadoki, kuhani, mfalme akamweka mahali pa Abiathari.

na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa jemadari wa jeshi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani;

Akaiacha maskani ya Shilo, Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu;

Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.

Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.

Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao.

Na katika wana wa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu, akaokoka mtu mmoja tu, aliyeitwa Abiathari, akamkimbilia Daudi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo