Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 15:14 - Swahili Revised Union Version

14 Lakini mahali pa juu hapakuondoshwa; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu kwa BWANA siku zake zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Lakini mahali pa juu pa kutambikia miungu hapakuharibiwa; hata hivyo, yeye alikuwa na moyo mwaminifu kwa Mwenyezi-Mungu maisha yake yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Lakini mahali pa juu pa kutambikia miungu hapakuharibiwa; hata hivyo, yeye alikuwa na moyo mwaminifu kwa Mwenyezi-Mungu maisha yake yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Lakini mahali pa juu pa kutambikia miungu hapakuharibiwa; hata hivyo, yeye alikuwa na moyo mwaminifu kwa Mwenyezi-Mungu maisha yake yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu maisha yake yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa bwana kikamilifu maisha yake yote.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 15:14
14 Marejeleo ya Msalaba  

Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.


Akaziendea dhambi zote za babaye, alizozifanya kabla yake; wala moyo wake haukuwa mkamilifu na BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi babaye.


Akaiendea njia yote ya Asa babaye; wala hakugeuka, akifanya yaliyo mema machoni pa BWANA. Lakini mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa dhabihu wakafukiza uvumba katika mahali pa juu.


Ila watu walikuwa wakitoa dhabihu katika mahali pa juu, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la BWANA, hata siku zile.


Sulemani naye akampenda BWANA, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.


Mioyo yenu na iwe kamili kwa BWANA, Mungu wetu, kuenenda katika sheria zake, na kuzishika amri zake, kama ilivyo leo.


Ila mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.


Walakini mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.


Ila mahali pa juu hapakuondolewa, nao watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.


maana aliziondoa madhabahu za kigeni, na mahali pa juu, akazivunja nguzo, akayakatakata maashera;


Tena akaondoa kutoka miji yote ya Yuda mahali pa juu na sanamu za jua; ufalme ukastarehe mbele yake.


Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.


Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, lakini si kwa moyo mkamilifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo