Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 9:2 - Swahili Revised Union Version

2 Naye alikuwa na mwana, aliyeitwa Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wote.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Kishi alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Shauli. Shauli alikuwa kijana mzuri, na hakuna mtu katika Israeli aliyelingana na Shauli kwa uzuri. Shauli alikuwa mrefu zaidi kuliko mtu yeyote katika nchi ya Israeli; watu wote walimfikia mabegani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Kishi alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Shauli. Shauli alikuwa kijana mzuri, na hakuna mtu katika Israeli aliyelingana na Shauli kwa uzuri. Shauli alikuwa mrefu zaidi kuliko mtu yeyote katika nchi ya Israeli; watu wote walimfikia mabegani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Alikuwa na mwana aliyeitwa Sauli, kijana aliyevutia sana, hakuna aliyelingana naye miongoni mwa Waisraeli; alikuwa mrefu kuliko watu wengine wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Alikuwa na mwana aliyeitwa Sauli, kijana anayevutia sana, hakuwepo aliyelingana naye miongoni mwa Waisraeli, alikuwa mrefu kuliko wengine wote.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Naye alikuwa na mwana, aliyeitwa Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wote.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 9:2
10 Marejeleo ya Msalaba  

wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wowote waliowachagua.

Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.

BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;

Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

Kisha akalileta kabila la Benyamini karibu, kulingana na jamaa zao; jamaa ya Wamatri ikachukuliwa kwa kura. Akaileta jamaa ya Wamatri karibu, mtu baada ya mtu; kisha Sauli, mwana wa Kishi, akachaguliwa kwa kura; lakini walipomtafuta hakuonekana.

Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja.

Na punda wa Kishi, baba yake Sauli, walikuwa wamepotea. Kishi akamwambia Sauli mwanawe, Haya basi, chukua mtumishi mmoja pamoja nawe, uondoke, uende ukawatafute punda hao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo