Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 23:2 - Swahili Revised Union Version

2 Basi Daudi akamwuliza BWANA, Je! Niende nikawapige hao Wafilisti? Naye BWANA akamwambia Daudi, Nenda ukawapige Wafilisti, na kuuokoa Keila.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, Daudi akamwomba Mwenyezi-Mungu shauri, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti hawa?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Ndiyo, nenda ukawashambulie Wafilisti na kuuokoa mji wa Keila.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, Daudi akamwomba Mwenyezi-Mungu shauri, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti hawa?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Ndiyo, nenda ukawashambulie Wafilisti na kuuokoa mji wa Keila.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, Daudi akamwomba Mwenyezi-Mungu shauri, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti hawa?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Ndiyo, nenda ukawashambulie Wafilisti na kuuokoa mji wa Keila.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 akauliza kwa Mwenyezi Mungu, akisema, “Je, niende na kuwashambulia hawa Wafilisti?” Mwenyezi Mungu akamjibu, “Nenda, washambulie Wafilisti na uuokoe Keila.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 akauliza kwa bwana, akisema, “Je, niende na kuwashambulia hawa Wafilisti?” bwana akamjibu, “Nenda, washambulie Wafilisti na uuokoe Keila.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Basi Daudi akamwuliza BWANA, Je! Niende nikawapige hao Wafilisti? Naye BWANA akamwambia Daudi, Nenda ukawapige Wafilisti, na kuuokoa Keila.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 23:2
17 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Niupandie mji wowote wa Yuda? BWANA akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni.


Basi Daudi akauliza kwa BWANA, akisema, Je! Nipande juu ya Wafilisti? Utawatia mkononi mwangu? Naye BWANA akamwambia Daudi, Panda; kwa kuwa hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.


Naye Daudi alipouliza kwa BWANA, alisema, Usipande; zunguka nyuma yao, ukawajie huko mbele ya miforsadi.


Daudi akamwuliza Mungu, akisema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye BWANA akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako.


Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.


Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.


Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za BWANA; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja naye, mkutano wote pia.


Basi wakuu hao wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa BWANA.


Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza BWANA, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao?


Basi wakazidi kumwuliza BWANA, Amebaki mtu asiyekuja huku bado? Naye BWANA akajibu, Tazama, amejificha kwenye mizigo.


Basi Sauli akataka shauri kwa Mungu, Je! Nishuke ili kuwafuatia Wafilisti? Je! Utawatia mikononi mwa Israeli? Lakini hakumjibu neno lolote siku ile.


Ila watu wake Daudi wakamwambia, Tazama, sisi tunaogopa hapa katika Yuda; je! Si zaidi tukienda Keila juu ya majeshi ya Wafilisti?


Basi Daudi akamwuliza BWANA tena, Naye BWANA akamjibu, akasema, Ondoka, ukashukie Keila; kwa kuwa nitawatia hao Wafilisti mikononi mwako.


Ikawa Abiathari, mwana wa Ahimeleki, alipomkimbilia Daudi huko Keila, alishuka na naivera mkononi mwake.


Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo