Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 20:13 - Swahili Revised Union Version

13 BWANA anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukutuma uende zako kwa amani; na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mwenyezi-Mungu na aniue ikiwa Shauli anakusudia kukudhuru, nami nisikutahadharishe ili uende mahali mbali ambapo utakuwa salama. Mwenyezi-Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mwenyezi-Mungu na aniue ikiwa Shauli anakusudia kukudhuru, nami nisikutahadharishe ili uende mahali mbali ambapo utakuwa salama. Mwenyezi-Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mwenyezi-Mungu na aniue ikiwa Shauli anakusudia kukudhuru, nami nisikutahadharishe ili uende mahali mbali ambapo utakuwa salama. Mwenyezi-Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, Mwenyezi Mungu na aniadhibu vikali zaidi iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. Mwenyezi Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, bwana na anishughulikie kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. bwana na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 BWANA anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukutuma uende zako kwa amani; na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 20:13
22 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.


Wakaja na watu wote wamshurutishe Daudi kula chakula, kukiwa bado mchana; lakini Daudi akaapa, akasema Mungu anitendee vivyo hivyo, na kuzidi, nikionja mkate, au kingine chochote kabla ya jua kutua.


lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwondolea Sauli, niliyemwondoa mbele yako.


Kama vile BWANA alivyokuwa pamoja na bwana wangu mfalme, kadhalika na awe pamoja na Sulemani, na kufanya kiti chake cha enzi kuwa kitukufu kuliko kiti cha enzi cha bwana wangu mfalme Daudi.


Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.


Ndipo Ben-hadadi akatuma kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu.


Sasa mwanangu, BWANA na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya BWANA, Mungu wako, kama alivyonena kuhusu habari zako.


ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye BWANA na awe pamoja nawe.


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.


Hakuna mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.


Pale utakapofia ndipo nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; BWANA anitende vivyo hivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.


Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yuko pamoja nawe.


Basi Sauli alipokwisha kuutwaa ufalme juu ya Israeli, alipigana na adui zake wote pande zote, juu ya Moabu, na juu ya wana wa Amoni, na juu ya Edomu, na juu ya wafalme wa Soba, na juu ya Wafilisti; na popote alipogeukia, akawashinda.


Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Nenda, na BWANA atakuwa pamoja nawe.


Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu BWANA alikuwa pamoja naye, ila amemwacha Sauli.


na mimi nitatoka nje na kusimama kando ya babangu huko shambani ulipo wewe, nami nitazungumza na babangu habari zako; nami nikiona neno lolote nitakuambia.


Naye Yonathani akamwambia Daudi, BWANA, Mungu wa Israeli, na awe shahidi; nitakapokuwa nimekwisha kumwuliza baba yangu, kama wakati huu kesho, au siku ya tatu, angalia, kama liko neno jema la kumfaa Daudi, je! Nisikupelekee habari na kukufunulia neno hili?


Nawe utanionesha fadhili za BWANA, ili nisife, si wakati huu tu maadamu mimi ni hai;


Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mmoja wa kiume, kutakapopambazuka.


Akamwuliza, Ni neno gani alilosema nawe? Nakusihi, usinifiche; Mungu akufanyie vivyo hivyo, na kuzidi, ukinificha lolote katika hayo yote BWANA aliyosema nawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo