Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 10:10 - Swahili Revised Union Version

10 Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii wakakutana naye; kisha Roho ya Mungu ikamjia kwa nguvu, naye akatabiri kati yao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Shauli na mtumishi wake walipofika huko Gibea, alilakiwa na kundi la manabii. Roho ya Mungu ilimjia kwa nguvu, na Shauli akaanza kutabiri pamoja na manabii hao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Shauli na mtumishi wake walipofika huko Gibea, alilakiwa na kundi la manabii. Roho ya Mungu ilimjia kwa nguvu, na Shauli akaanza kutabiri pamoja na manabii hao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Shauli na mtumishi wake walipofika huko Gibea, alilakiwa na kundi la manabii. Roho ya Mungu ilimjia kwa nguvu, na Shauli akaanza kutabiri pamoja na manabii hao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Walipofika Gibea, akakutana na kundi la manabii. Roho wa Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akajiunga nao katika kutoa unabii kwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Walipofika Gibea, akakutana na kundi la manabii. Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akajiunga nao katika kutoa unabii kwao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii wakakutana naye; kisha Roho ya Mungu ikamjia kwa nguvu, naye akatabiri kati yao.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 10:10
7 Marejeleo ya Msalaba  

Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.

Roho ya BWANA ikamjia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kuenda vitani, naye BWANA akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu.

Na Roho ya Mungu ikamjia Sauli kwa nguvu, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana.

Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.

Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya kulingana na yale yaliyo katika moyo wangu na katika akili yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo