Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wafilipi 4:7 - Neno: Maandiko Matakatifu

7 Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

7 Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 4:7
43 Marejeleo ya Msalaba  

Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana chochote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa bwana. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya bwana ni nguvu zenu.”


“Mjue sana Mungu ili uwe na amani, ndipo mema yatakapokujia.


Lakini kama akinyamaza kimya, ni nani awezaye kumhukumu? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumwona? Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa,


bwana huwapa watu wake nguvu; bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.


Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye bwana; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: lakini nao wasirudie upumbavu.


Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda.


Usimwache hekima naye atakuweka salama; mpende, naye atakulinda.


Wakati utembeapo, yatakuongoza; wakati ulalapo, yatakulinda; wakati uamkapo, yatazungumza nawe.


bwana, unaamuru amani kwa ajili yetu, yale yote tuliyoweza kuyakamilisha ni wewe uliyetenda kwa ajili yetu.


Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini wewe.


Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, ninaleta mafanikio na kusababisha maafa. Mimi, bwana, huyatenda haya yote.


Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu, amani yako ingekuwa kama mto, haki yako kama mawimbi ya bahari.


“Hakuna amani kwa waovu,” asema bwana.


“Baada ya kumkabidhi Baruku mwana wa Neria hii hati ya kununulia, nilimwomba bwana:


“ ‘Hata hivyo, nitauletea afya na uponyaji, nitawaponya watu wangu na kuwafanya wafurahie amani tele na salama.


bwana akugeuzie uso wake na kukupa amani.” ’


ili kuwaangazia wale waishio gizani na katika uvuli wa mauti, kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”


“Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”


Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.


Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”


Kwa wote walioko Rumi wapendwao na Mungu na kuitwa kuwa watakatifu: Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi.


Kwa maana Ufalme wa Mwenyezi Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho wa Mwenyezi Mungu.


Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho wa Mwenyezi Mungu.


Kwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Isa Al-Masihi,


Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani.


tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Al-Masihi,


Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, mkafarijike, kuweni wa nia moja, kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.


Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu.


Waraka wa Paulo na Timotheo, watumishi wa Al-Masihi Isa: Kwa watakatifu wote katika Al-Masihi Isa walioko Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi:


Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi.


Naye Mungu wangu atawajaza ninyi na kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Al-Masihi Isa.


Msalimuni kila mtakatifu katika Al-Masihi Isa. Ndugu walioko pamoja nami wanawasalimu.


Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.


Amani ya Al-Masihi na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.


Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Bwana awe nanyi nyote.


Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Isa, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo,


Yuda, mtumwa wa Isa Al-Masihi, na nduguye Yakobo: Kwa wale walioitwa, wapendwa katika Mungu Baba na kuhifadhiwa salama ndani ya Isa Al-Masihi:


Yohana, kwa makundi saba ya waumini yaliyoko Asia: Neema na amani iwe kwenu kutoka kwake aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, na kutoka kwa wale roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi,


“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo