Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wafilipi 1:15 - Neno: Maandiko Matakatifu

15 Ni kweli kwamba wengine wanamhubiri Al-Masihi kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana, lakini wengine wanamhubiri Al-Masihi kwa nia njema.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kweli, baadhi yao wanamhubiri Kristo kwa sababu wana wivu na ni watu wagomvi; lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia nzuri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kweli, baadhi yao wanamhubiri Kristo kwa sababu wana wivu na ni watu wagomvi; lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia nzuri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kweli, baadhi yao wanamhubiri Kristo kwa sababu wana wivu na ni watu wagomvi; lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia nzuri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Ni kweli kwamba wengine wanamhubiri Al-Masihi kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana, lakini wengine wanamhubiri Al-Masihi kwa nia njema.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

15 Kweli, baadhi yao wanamhubiri Kristo kwa sababu wana wivu na ni watu wagomvi; lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia nzuri.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 1:15
22 Marejeleo ya Msalaba  

“Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao.


Ninyi mnajua ule ujumbe uliotumwa kwa Israeli, ukitangaza habari njema za amani kwa Isa Al-Masihi. Yeye ni Bwana wa wote.


Lakini baadhi yao walikuwepo watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakiwahubiria habari njema za Bwana Isa.


Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema kwamba Isa ndiye Al-Masihi.


Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la Maandiko, akamweleza habari njema za Isa.


Filipo akateremkia mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Al-Masihi.


Papo hapo akaanza kuhubiri kwenye masinagogi kwamba “Isa Al-Masihi ni Mwana wa Mungu.”


Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.


Lakini sisi tunamhubiri Al-Masihi aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi.


Kama nikitoa mali yote niliyo nayo na kama nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.


Kwa kuwa Isa Al-Masihi, Mwana wa Mungu, ambaye tulimhubiri kwenu: Mimi, Silvano na Timotheo, hakuwa “Ndiyo” na “Siyo,” bali kwake yeye siku zote ni “Ndiyo.”


Watu kama hao ni mitume wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu, wanaojigeuza waonekane kama mitume wa Al-Masihi.


Kwa kuwa nina hofu ya kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko.


Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Isa Al-Masihi kuwa ni Bwana na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Isa.


Lakini kwa sababu ya ndugu wa uongo ambao walijiingiza kwa siri katikati yetu ili kupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Al-Masihi Isa, wapate kututia utumwani,


Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza wala kujivuna, bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake.


Bila shaka yoyote, siri ya utauwa ni kubwa: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, akathibitishwa kuwa na haki katika Roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo