Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 5:48 - Neno: Maandiko Matakatifu

48 Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

48 Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

48 Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

48 Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

48 Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

48 Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

48 Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:48
25 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.


“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.


Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.


Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi wenyewe kwa kiumbe chochote kile kiendacho juu ya ardhi.


“Sema na kusanyiko lote la Israeli na uwaambie: ‘Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi, bwana Mwenyezi Mungu wenu, ni mtakatifu.


Mtakuwa watakatifu kwangu, kwa sababu Mimi, bwana, ni mtakatifu, nami nimewatenga kutoka mataifa kuwa wangu mwenyewe.


Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.


Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo?


Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.


Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, ila yule aliyehitimu aweza kuwa kama mwalimu wake.


Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, mkafarijike, kuweni wa nia moja, kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.


Tunafurahi wakati wowote sisi tunapokuwa dhaifu, lakini ninyi mkawa na nguvu. Nayo maombi yetu ni kwamba mpate kuwa wakamilifu.


Wapenzi, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu.


Kwa sababu hii, mimi Paulo, mfungwa wa Al-Masihi Isa kwa ajili yenu ninyi watu wa Mataifa:


Kamwe msilaumiwe mbele za bwana Mwenyezi Mungu wenu.


Mtii bwana Mwenyezi Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”


Yeye ndiye tunayemtangaza, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja akiwa amekamilika katika Al-Masihi.


Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Al-Masihi Isa, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mwenyezi Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti.


Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote.


Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo