Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 5:39 - Neno: Maandiko Matakatifu

39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

39 Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:39
24 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Sedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa bwana alipita njia gani alipotoka kwangu ili kusema nawe?”


Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, na kuungana pamoja dhidi yangu.


Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!” Mngojee bwana, naye atakuokoa.


Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”


Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao, mashavu yangu wale wang’oao ndevu zangu; sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha na kutemewa mate.


Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu.


“ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi bwana.


Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi, kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. Watampiga mtawala wa Israeli shavuni kwa fimbo.


Kama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia.


Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?”


Mafarisayo na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato.


Isa akamjibu akasema, “Kama nimesema jambo baya, shuhudia huo ubaya niliousema. Lakini kama nimesema yaliyo kweli, mbona umenipiga?”


Huko kuwa na mashtaka miongoni mwenu ina maana kwamba tayari ni kushindwa kabisa. Kwa nini msikubali kutendewa mabaya? Kwa nini msikubali kunyang’anywa?


Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.


Katika kushindana kwenu dhidi ya dhambi, bado hamjapigana kiasi cha kumwaga damu yenu.


Mmewahukumu na kuwaua watu wenye haki, waliokuwa hawapingani nanyi.


Msilipe ovu kwa ovu, au jeuri kwa jeuri, bali barikini, kwa maana hili ndilo mliloitiwa ili mpate kurithi baraka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo