Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mathayo 5:20 - Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo na walimu wa Torati, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo na walimu wa Torati, kamwe hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Mathayo 5:20
24 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi juu ya chachu ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

“Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi.

Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti, basi kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni.

“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mwenyezi Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”

Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu.”

“Ole wenu, kwa sababu ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”

Wakati huo, umati mkubwa wa watu maelfu, walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Isa akaanza kuzungumza kwanza na wanafunzi wake, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao.

Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mwenyezi Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”

Ikiwa huduma ile inayowahukumu wanadamu ina utukufu, je, ile huduma iletayo haki haitakuwa ya utukufu zaidi?

Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya.

Nami nionekane mbele zake bila kuwa na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika Al-Masihi, haki ile itokayo kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya imani.

Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao hakuna mtu atakayemwona Bwana.

Lakini kitu kichafu hakitaingia humo kamwe, wala mtu yeyote atendaye mambo ya aibu au ya udanganyifu. Bali watakaoingia humo ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo