Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wafilipi 4:8 - Neno: Bibilia Takatifu

8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

8 Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 4:8
67 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Mwenyezi Mungu atimize ahadi yake kwa Ibrahimu.”


Sauli na Yonathani: maishani walipendwa na kuneemeka, na katika kifo hawakutengana. Walikuwa wepesi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba.


Mungu wa Israeli alinena, mwamba wa Israeli akaniambia: ‘Mtu anatawala watu kwa haki, wakati anapotawala akiwa na hofu ya Mungu,


“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonesha upendeleo kwa waovu?


Mwenyezi Mungu huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake.


Mke mwenye tabia nzuri ni taji la mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.


Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Mwenyezi Mungu; mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.


Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, wamebarikiwa watoto wake baada yake.


Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.


“Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri, lakini wewe umewapita wote.”


Mpe thawabu anayostahili, nazo kazi zake na zimletee sifa kwenye lango la mji.


Kinywa chake chenyewe ni utamu, kwa ujumla yeye ni wa kupendeza. Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki yangu, ee binti za Yerusalemu.


Mapito ya wenye haki ni nyoofu. Ewe uliye Mwenye Haki, waisawazisha njia ya mtu mnyofu.


Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode kwake. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonesha upendeleo.


kwa sababu Herode alimwogopa Yahya akijua kwamba ni mtu mwenye haki na mtakatifu, hivyo akamlinda. Herode alifadhaika sana alipomsikia Yohana, lakini bado alipenda kumsikiliza.


Isa akawaambia, “Ninyi mnajionesha kuwa wenye haki mbele za wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu ni machukizo.


Basi huko Yerusalemu kulikuwa mtu mmoja aliyeitwa Simeoni, aliyekuwa mwenye haki na mcha Mungu. Alikuwa akitazamia faraja ya Israeli, na Roho Mtakatifu wa Mungu alikuwa juu yake.


Basi kulikuwa na mtu mmoja mwema na mwenye haki, jina lake Yusufu. Yeye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wayahudi,


Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake.


Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani mwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.”


“Mtu mmoja mcha Mungu, jina lake Anania, alikuja kuniona. Alizishika sana sheria zetu, na aliheshimiwa sana na Wayahudi walioishi huko Dameski.


Kwa hiyo ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu wa Mungu na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi kazi hii,


Basi na tuenende kwa adabu kama inavyopasa wakati wa mchana, si kwa kufanya karamu za ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.


Kwa kuwa watawala hawawatishi watu wale wanaotenda mema bali wale wanaotenda mabaya. Je, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Basi tenda lile lililo jema naye atakusifu.


Kwa sababu mtu yeyote anayemtumikia Al-Masihi kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.


Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho wa Mungu, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu kama huyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu.


Kwa hiyo msihukumu jambo lolote kabla ya wakati wake. Ngojeni hadi Bwana Isa atakapokuja. Yeye atayaleta nuruni mambo yale yaliyofichwa gizani, na kuweka wazi nia za mioyo ya wanadamu. Wakati huo kila mmoja atapokea sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.


Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda kosa lolote, si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda hilo jaribio, bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaonekana kuwa tumeshindwa.


katika utukufu na katika kudharauliwa, katika sifa mbaya na katika sifa nzuri; tukionekana kama wadanganyaji, lakini tukiwa wakweli;


Nasi tunamtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa na makundi yote ya waumini kwa huduma yake ya kuhubiri Injili.


Kwa kuwa tunakusudia kufanya kile kilicho haki, si machoni mwa Bwana Isa peke yake, bali pia machoni mwa wanadamu.


Lakini tunda la Roho wa Mungu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.


(kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli),


Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani,


Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa.


Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana Isa! Mimi kuwaandikia mambo yale yale hakuniudhi, kwa maana ni kinga kwa ajili yenu.


Nendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.


ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote.


kwa ajili ya wafalme na wale wote walio katika mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu.


Vivyo hivyo, wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasio wasingiziaji, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo.


Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia.


Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi.


awe ameshuhudiwa kwa matendo yake mema, aliyewalea watoto wake vizuri, aliye mkarimu, aliyewanawisha watakatifu miguu, aliyewasaidia wenye shida na aliyejitolea kwa ajili ya matendo mema ya kila namna.


nao wanawake wazee uwatendee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako, katika usafi wote.


Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.


Ndiye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe kutoka uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani wale walio na juhudi katika kutenda mema.


Wafundishe wazee kuwa na kiasi, wastahivu, wenye busara na wanyofu katika imani, upendo na saburi.


Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uoneshe uadilifu, utaratibu,


Watu wetu hawana budi kujifunza kutenda mema, ili waweze kuyakimu mahitaji ya kila siku, wasije wakaishi maisha yasiyokuwa na matunda.


Maana baba zetu wa kale walipongezwa kwa haya.


Tuombeeni. Tuna hakika kuwa tunayo dhamiri safi na shauku ya kuishi kwa uadilifu kwa kila njia.


Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu, Baba yetu, ndiyo hii: ni kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.


Lakini hekima inayotoka mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki.


Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.


Kuweni na mwenendo mzuri mbele ya watu wasiomjua Mungu, ili kama wanawasingizia kuwa watenda mabaya, wayaone matendo yenu mema nao wamtukuze Mungu siku atakapokuja kwetu.


Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi.


Wapendwa, huu ndio waraka wangu wa pili ninaowaandikia. Katika nyaraka hizi mbili ninajaribu kuziamsha nia zenu safi kwa mawazo makamilifu.


Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli.


Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.


Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni.


Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo