Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 4:4 - BIBLIA KISWAHILI

4 Muwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi; tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi; tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi; tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Katika hasira yako, usitende dhambi. Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu, mkiichunguza mioyo yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

4 Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi; tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza.

Tazama sura Nakili




Zaburi 4:4
17 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.


Wakuu wameniudhi bure, Ila moyo wangu unakaa kwa kicho cha maneno yako.


Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.


Mtumikieni BWANA kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka.


Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu.


Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.


Nchi yote na imwogope BWANA, Wote wakaao duniani na wamche.


Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.


Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Ninakutafakari usiku kucha.


Nanena na moyo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu naipeleleza.


Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.


Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.


Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.


Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.


Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.


Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.


Muwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo