Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yohana 1:4 - Biblia Habari Njema

4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ndani yake kulikuwa na uzima, nao huo uzima ulikuwa nuru ya watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.

Tazama sura Nakili




Yohana 1:4
30 Marejeleo ya Msalaba  

Watu waovu hutegemea mali zao, hujisifia wingi wa utajiri wao.


Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu; yeye hutuneemesha na kutujalia fahari. Hawanyimi chochote kilicho chema, wale waishio kwa unyofu.


“Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu, nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui. Mbele yao giza nitaligeuza kuwa mwanga, na mahali pa kuparuza patakuwa laini. Huo ndio mpango wangu wa kufanya, nami nitautekeleza.


Lakini kwa ajili yenu nyinyi mnaonicha, uwezo wangu wa kuokoa utawachomozea kama jua lililo na nguvu za kuponya kwenye mionzi yake. Mtatoka mkirukaruka kama ndama watokapo zizini mwao.


Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!”


Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli.”


Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi;


Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.


Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniamini wasibaki gizani.


Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na ukweli na uhai. Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu.


Na hukumu yenyewe ndiyo hii: Mwanga umekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko mwanga, kwani matendo yao ni maovu.


Kama vile Baba huwafufua wafu na kuwapa uhai, vivyo hivyo naye Mwana huwapa uhai wale anaopenda.


Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo pia alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai.


Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, “Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uhai.”


Wakati ningali ulimwenguni, mimi ni mwanga wa ulimwengu.”


yaani ilimpasa Kristo ateseke na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, ili atangaze kwamba mwanga wa ukombozi unawaangazia sasa watu wote, Wayahudi na pia watu wa mataifa mengine.”


Maana Maandiko yasema: “Mtu wa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbe mwenye uhai;” lakini Adamu wa mwisho ni Roho awapaye watu uhai.


na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: “Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka kwa wafu, naye Kristo atakuangaza.”


Uhai wenu halisi ni Kristo, na wakati atakapotokea ndipo nanyi pia mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.


Habari hii yahusu Neno la uhai lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu wenyewe.


Uhai huo ulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasema habari zake na kuwaambieni juu ya uhai huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu.


Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uhai wa milele, na uhai huo uko kwa Bwana.


Kisha malaika akanionesha mto wa maji ya uhai maangavu kama kioo, yakitoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo.


“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”


Tufuate:

Matangazo


Matangazo