Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wafilipi 2:14 - Biblia Habari Njema

14 Fanyeni kila kitu bila kunungunika na bila ubishi,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

14 Fanyeni kila kitu bila kunungunika na bila ubishi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Fanyeni kila kitu bila kunung'unika na bila ubishi,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Fanyeni mambo yote bila kunung’unika wala kushindana,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Fanyeni mambo yote bila kunung’unika wala kushindana,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano,

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

14 Fanyeni kila kitu bila kunungunika na bila ubishi,

Tazama sura Nakili




Wafilipi 2:14
36 Marejeleo ya Msalaba  

Walinungunika mahemani mwao, wala hawakumsikiliza Mwenyezi-Mungu.


Kiburi husababisha tu ugomvi, lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima.


“Kundi hili la watu waovu litaendelea kuninungunikia mpaka lini? Nimechoka na haya manunguniko ya Waisraeli juu yangu!


Wakazipokea fedha zao, wakaanza kumnungunikia yule bwana.


Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi cha dinari 300, wakapewa maskini!” Wakamkemea huyo mama.


Walipowafikia wale wanafunzi wengine, waliona umati mkubwa wa watu hapo. Na baadhi ya waalimu wa sheria walikuwa wanajadiliana nao.


Mafarisayo na waalimu wa sheria wakawanungunikia wanafunzi wake wakisema: “Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?”


Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, na baada ya Paulo na Barnaba kujadiliana nao, ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja na waumini kadhaa wa lile kanisa la Antiokia waende Yerusalemu kuwaona wale mitume na wazee kuhusu jambo hilo.


Basi, kukatokea ubishi mkali kati yao, wakaachana. Barnaba akamchukua Marko, wakapanda meli kwenda Kupro.


Baada ya majadiliano marefu, Petro alisimama, akasema, “Ndugu zangu, nyinyi mnafahamu kwamba hapo awali Mungu alipenda kunichagua mimi miongoni mwenu nitangaze Habari Njema kwa watu wa mataifa, wapate kusikia na kuamini.


Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manunguniko kati ya waumini walioongea Kigiriki na wale walioongea Kiebrania. Wale walioongea Kigiriki walinungunika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.


Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote.


Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi.


Ndugu zangu, nawasihi mwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao,


Wala msinungunike kama baadhi yao walivyonungunika, wakaangamizwa na Mwangamizi!


Naogopa, huenda nitakapokuja kwenu nitawakuta katika hali nisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali msiyoipenda. Naogopa huenda kukawa na ugomvi, wivu, uhasama, ubishi, masengenyo, kunongona, majivuno na fujo kati yenu.


Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana kama wanyama, jihadharini msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe!


Basi, tusijivune, tusichokozane wala kuoneana wivu.


Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.


Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amani kati yenu.


Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.


Jitahidini kuishi kwa amani na watu wote. Ishini maisha ya utakatifu, kwa sababu hakuna mtu atakayemwona Bwana bila ya maisha kama hayo.


Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki.


Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.


Ndugu zangu, msinung'unikiane nyinyi kwa nyinyi msije mkahukumiwa na Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia.


Ajiepushe na uovu, atende mema, atafute amani na kuizingatia.


Muwe na ukarimu nyinyi kwa nyinyi bila kunung'unika.


Watu hawa hunung'unika daima, hulalamika, hufuata tamaa zao mbaya, hujigamba na kuwasifu watu wengine mno kwa faida yao wenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo