Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.
Zekaria 3:6 - Swahili Revised Union Version Kisha malaika wa BWANA akamshuhudia Yoshua, akisema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwonya kuhani mkuu Yoshua, akamwambia, Biblia Habari Njema - BHND Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwonya kuhani mkuu Yoshua, akamwambia, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwonya kuhani mkuu Yoshua, akamwambia, Neno: Bibilia Takatifu Malaika wa Mwenyezi Mungu akamwamuru Yoshua: Neno: Maandiko Matakatifu Malaika wa bwana akamwamuru Yoshua: BIBLIA KISWAHILI Kisha malaika wa BWANA akamshuhudia Yoshua, akisema, |
Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.
Kwa maana niliwashuhudia sana baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, hata leo, nikiamka mapema na kuwashuhudia, nikisema, Itiini sauti yangu.
Naam, alishindana na malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;
Kisha akanionesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kulia ili kushindana naye.
Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa BWANA akasimama karibu.
BWANA wa majeshi asema hivi, Ikiwa utaenda katika njia zangu, na kushika maagizo yangu, basi utaihukumu nyumba yangu, na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa haki ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.