Katika siku zake, Farao Neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana na mfalme wa Ashuru, akafika mto Frati; naye mfalme Yosia akaenda kupigana naye; naye mfalme wa Misri akamwua huko Megido, hapo alipoonana naye.
Zekaria 12:11 - Swahili Revised Union Version Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu mjini Yerusalemu kama maombolezo ya kumwombolezea Hadad-rimoni katika mbuga za Megido. Biblia Habari Njema - BHND Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu mjini Yerusalemu kama maombolezo ya kumwombolezea Hadad-rimoni katika mbuga za Megido. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu mjini Yerusalemu kama maombolezo ya kumwombolezea Hadad-rimoni katika mbuga za Megido. Neno: Bibilia Takatifu Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido. BIBLIA KISWAHILI Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido. |
Katika siku zake, Farao Neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana na mfalme wa Ashuru, akafika mto Frati; naye mfalme Yosia akaenda kupigana naye; naye mfalme wa Misri akamwua huko Megido, hapo alipoonana naye.
Lakini Yosia hakukubali kumwachia, akajibadilisha apate kupigana naye, asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani kwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido.
Basi watumishi wake wakamtoa garini, wakamtia katika gari la pili alilokuwa nalo, wakamleta Yerusalemu; naye akafa, akazikwa makaburini mwa babaze. Watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakamlilia Yosia.
Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na makabila yote ya dunia yataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.