Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako;
Zaburi 7:3 - Swahili Revised Union Version BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu! Kama nimetenda moja ya mambo haya: Kama nimechafua mikono yangu kwa ubaya, Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu! Kama nimetenda moja ya mambo haya: Kama nimechafua mikono yangu kwa ubaya, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu! Kama nimetenda moja ya mambo haya: kama nimechafua mikono yangu kwa ubaya, Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu, Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu, BIBLIA KISWAHILI BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu, |
Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako;
Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamepanga kunishambulia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu.
Mungu, Mungu BWANA, naam, Mungu, Mungu BWANA, yeye anajua, na Israeli naye atajua; kama ni katika uasi, au kama ni katika kosa juu ya BWANA, usituokoe hivi leo;
Basi, unitendee mema mimi mtumishi wako; kwa sababu umenitia mimi mtumishi wako katika agano la BWANA pamoja nawe, lakini ikiwa mna uovu moyoni mwangu, uniue wewe mwenyewe; kwa nini kunileta kwa baba yako?
Sauli akamwuliza, Mbona mmefanya fitina juu yangu, wewe na mwana wa Yese? Kwa maana umempa mikate, na upanga, nawe umemwuliza Mungu kwa ajili yake, ili aniasi na kunivizia kama hivi leo?
hata ninyi nyote mkanifitinia, wala hapana mtu anifunuliaye habari hii mwanangu afanyapo agano na mwana wa Yese, wala hapana mmoja wenu anayenisikitikia, wala kunifunulia ya kuwa mwanangu amemchochea mtumishi wangu, anivizie kama hivi leo?
Tena, baba yangu, tazama, tafadhali, tazama upindo wa vazi lako mkononi mwangu; maana ikiwa nimeukata upindo wa vazi lako, nisikuue, ujue, na kuona ya kuwa hakuna uovu wala kosa mkononi mwangu, wala sikukukosa neno; ingawa wewe unaniwinda roho yangu ili kuikamata.
Daudi akamwambia Sauli, Kwa nini unasikiliza maneno ya watu wasemao, Tazama, Daudi anataka kukudhuru?