Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini?
Yoshua 4:20 - Swahili Revised Union Version Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yoshua akayasimika yale mawe kumi na mawili ambayo waliyachukua kutoka mtoni Yordani, huko Gilgali. Biblia Habari Njema - BHND Yoshua akayasimika yale mawe kumi na mawili ambayo waliyachukua kutoka mtoni Yordani, huko Gilgali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yoshua akayasimika yale mawe kumi na mawili ambayo waliyachukua kutoka mtoni Yordani, huko Gilgali. Neno: Bibilia Takatifu Naye Yoshua akayasimamisha huko Gilgali yale mawe kumi na mbili waliyokuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani. Neno: Maandiko Matakatifu Naye Yoshua akayasimamisha huko Gilgali yale mawe kumi na mawili ambayo walikuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani. BIBLIA KISWAHILI Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali. |
Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini?
kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende na mawe hayo, mkayaweke mahali pale kambini ambapo mtalala usiku huu.
Basi wana wa Israeli walifanya vile vile kama Yoshua alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, kama BWANA alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya makabila ya wana wa Israeli; wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayarundika huko.