Yoshua 3:9 - Swahili Revised Union Version Basi Yoshua akawaambia wana wa Israeli, Njoni huku, mkayasikie maneno ya BWANA, Mungu wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Yoshua akawaambia Waisraeli: “Njoni karibu mpate kusikia maneno ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Biblia Habari Njema - BHND Kisha Yoshua akawaambia Waisraeli: “Njoni karibu mpate kusikia maneno ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Yoshua akawaambia Waisraeli: “Njoni karibu mpate kusikia maneno ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” Neno: Bibilia Takatifu Yoshua akawaambia Waisraeli, “Njooni hapa msikilize maneno ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Neno: Maandiko Matakatifu Yoshua akawaambia Waisraeli, “Njooni hapa msikilize maneno ya bwana Mwenyezi Mungu wenu. BIBLIA KISWAHILI Basi Yoshua akawaambia wana wa Israeli, Njoni huku, mkayasikie maneno ya BWANA, Mungu wenu. |
Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.
Yoshua akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na Mwamori, na Myebusi.
Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la Agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani.