Yoshua 23:11 - Swahili Revised Union Version Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, muwe waangalifu sana kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, muwe waangalifu sana kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, muwe waangalifu sana kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo kuweni waangalifu sana kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo kuweni waangalifu sana kumpenda bwana Mwenyezi Mungu wenu. BIBLIA KISWAHILI Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu. |
Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.
kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.
Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yoyote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.
Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.
Lakini mkirudi nyuma kwa njia yoyote na kushikamana na mabaki ya mataifa, yaani, mataifa haya yaliyobaki kati yenu, na kuoana nao, na kuingia kwao, nao kuingia kwenu;