Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kulia, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;
Yoshua 21:9 - Swahili Revised Union Version Kisha wakawapa katika kabila la wana wa Yuda, na katika kabila la wana wa Simeoni, miji hii iliyotajwa hapa kwa majina; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yafuatayo ni majina ya miji kutoka kwenye maeneo ya kabila la Yuda na Simeoni ambayo ilitolewa kwa Biblia Habari Njema - BHND Yafuatayo ni majina ya miji kutoka kwenye maeneo ya kabila la Yuda na Simeoni ambayo ilitolewa kwa Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yafuatayo ni majina ya miji kutoka kwenye maeneo ya kabila la Yuda na Simeoni ambayo ilitolewa kwa Neno: Bibilia Takatifu Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina Neno: Maandiko Matakatifu Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina BIBLIA KISWAHILI Kisha wakawapa katika kabila la wana wa Yuda, na katika kabila la wana wa Simeoni, miji hii iliyotajwa hapa kwa majina; |
Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kulia, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;
Tena wakawapa kwa kura miji hiyo iliyotajwa majina yake, katika kabila la wana wa Yuda, na katika kabila la wana wa Simeoni, na katika kabila la wana wa Benyamini.
Na chini yake walikuwa Edeni, na Minyamini, na Yeshua, na Shemaya, na Amaria, na Shekania, mijini mwa makuhani, kwa walivyoaminiwa, ili kuwagawia ndugu zao kwa zamu, wakuu na wadogo sawasawa;
nayo ilikuwa kwa ajili ya wana wa Haruni, wa jamaa ya Wakohathi, waliokuwa wa wana wa Lawi; kwa kuwa kura ya kwanza ilikuwa ni yao.
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni, na katika kabila la Benyamini.
Kisha wana wa Israeli waliwapa Walawi kwa kura miji hiyo pamoja na mbuga zake za malisho, kama BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa.