Yoshua 21:6 - Swahili Revised Union Version Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa ukoo wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase huko Bashani. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa ukoo wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase huko Bashani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa ukoo wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase huko Bashani. Neno: Bibilia Takatifu Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na tatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani. Neno: Maandiko Matakatifu Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani. BIBLIA KISWAHILI Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani. |
Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, kulingana na jamaa zao, katika kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika kabila la Manase waliokaa Bashani.
Kisha Wakohathi wengine waliosalia walipata kwa kura miji kumi katika jamaa za kabila la Efraimu, na katika kabila la Dani, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase.
Na wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao walipata miji kumi na miwili katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi, na katika kabila la Zabuloni.