Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.
Yoshua 21:41 - Swahili Revised Union Version Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arubaini na minane, pamoja na mbuga zake za malisho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa arubaini na minane pamoja na mbuga zao za malisho. Biblia Habari Njema - BHND Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa arubaini na minane pamoja na mbuga zao za malisho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa arubaini na minane pamoja na mbuga zao za malisho. Neno: Bibilia Takatifu Miji yote ya Walawi katika eneo lililomilikiwa na Waisraeli ilikuwa arobaini na nane, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji. Neno: Maandiko Matakatifu Miji yote ya Walawi katika eneo lililoshikwa na Waisraeli lilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho. BIBLIA KISWAHILI Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arobaini na minane, pamoja na mbuga zake za malisho. |
Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.
Watamfundisha Yakobo hukumu zako, Na Israeli torati yako, Wataweka uvumba mbele zako, Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako.
Basi wana wa Israeli wakawapa Walawi miji hii, pamoja na mbuga zake za malisho, katika urithi wao, sawasawa na hiyo amri ya BWANA.
Miji hiyo yote ilikuwa ni miji ya wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao, ni hizo jamaa za Walawi zilizosalia; na kura yao ilikuwa ni miji kumi na miwili.
Miji hiyo kila mmoja ulikuwa pamoja na mbuga zake za malisho, yaliyouzunguka pande zote; ndivyo ilivyokuwa katika miji hiyo yote.