Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu.
Yoshua 21:33 - Swahili Revised Union Version Miji yote ya Wagershoni kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na mbuga zake za malisho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jumla ya miji ya jamaa mbalimbali za ukoo wa Gershoni ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho. Biblia Habari Njema - BHND Jumla ya miji ya jamaa mbalimbali za ukoo wa Gershoni ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jumla ya miji ya jamaa mbalimbali za ukoo wa Gershoni ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho. Neno: Bibilia Takatifu Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na tatu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji. Neno: Maandiko Matakatifu Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho. BIBLIA KISWAHILI Miji yote ya Wagershoni kwa kufuata jamaa zao ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na mbuga zake za malisho. |
Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu.
Tena jamaa za wana wa Merari, hao Walawi waliosalia, katika kabila la Zabuloni, Yokneamu pamoja na mbuga zake za malisho, na Karta pamoja na mbuga zake za malisho,
Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani.