na katika kabila la Naftali; Kedeshi katika Galilaya pamoja na viunga vyake, na Hamothi pamoja na viunga vyake, na Kiriathaimu pamoja na viunga vyake.
Yoshua 21:32 - Swahili Revised Union Version Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Katika eneo la kabila la Naftali walipewa Kedeshi, mji wa kukimbilia usalama ulioko huko Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mitatu. Biblia Habari Njema - BHND Katika eneo la kabila la Naftali walipewa Kedeshi, mji wa kukimbilia usalama ulioko huko Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mitatu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Katika eneo la kabila la Naftali walipewa Kedeshi, mji wa kukimbilia usalama ulioko huko Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mitatu. Neno: Bibilia Takatifu Kutoka kabila la Naftali, walipewa: Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji mitano. Neno: Maandiko Matakatifu Kutoka kabila la Naftali walipewa, Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji mitano. BIBLIA KISWAHILI Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu. |
na katika kabila la Naftali; Kedeshi katika Galilaya pamoja na viunga vyake, na Hamothi pamoja na viunga vyake, na Kiriathaimu pamoja na viunga vyake.
Nao wakaweka Kedeshi katika Galilaya katika nchi ya vilima ya Naftali, na Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-arba (ndio Hebroni) katika nchi ya vilima ya Yuda.
na Helkathi pamoja na mbuga zake za malisho, na Rehobu pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne.
Miji yote ya Wagershoni kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na mbuga zake za malisho.
Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: “Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori”.