Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali.
Yoshua 19:39 - Swahili Revised Union Version Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Naftali; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema - BHND Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Naftali; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Naftali; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. Neno: Bibilia Takatifu Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Naftali, kufuatana na koo zao. Neno: Maandiko Matakatifu Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo. BIBLIA KISWAHILI Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake. |
Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali.
Na mpakani mwa Asheri, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Naftali, fungu moja.
Ironi, Migdal-eli, Horemu, Bethanathi na Beth-shemeshi; miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.
Kisha sehemu ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao.