Yoshua 11:7 - Swahili Revised Union Version Basi Yoshua akaenda, na watu wote wa vita pamoja naye, ili kupigana nao hapo penye maji ya Meromu ghafla; wakawashambulia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, ghafla kwenye chemchemi ya Meromu Yoshua pamoja na jeshi lake lote akawatokea na kuwashambulia. Biblia Habari Njema - BHND Basi, ghafla kwenye chemchemi ya Meromu Yoshua pamoja na jeshi lake lote akawatokea na kuwashambulia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, ghafla kwenye chemchemi ya Meromu Yoshua pamoja na jeshi lake lote akawatokea na kuwashambulia. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Yoshua na jeshi lake lote wakaja dhidi yao ghafula kwenye Maji ya Meromu na kuwashambulia, Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Yoshua pamoja na jeshi lake lote wakaja dhidi yao ghafula kwenye Maji ya Meromu kuwashambulia, BIBLIA KISWAHILI Basi Yoshua akaenda, na watu wote wa vita pamoja naye, ili kupigana nao hapo penye maji ya Meromu ghafla; wakawashambulia. |
BWANA akamwambia Yoshua, Wewe usiogope kwa ajili ya hao; kwani kesho wakati kama huu nitawatoa wakiwa wameuawa wote mbele ya Israeli; utawakata farasi wao, na magari yao utayateketeza kwa moto.
BWANA akawatia mkononi mwa Israeli, nao wakawapiga, na kuwafukuza mpaka kufikia Sidoni ulio mkuu, tena hadi kufika Misrefoth-maimu, tena hata kufikia bonde la Mispa upande wa mashariki; wakawaua wote, wasibakize hata mtu mmoja