Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu chochote kipumzikacho;
Yoshua 11:11 - Swahili Revised Union Version Nao wakawapiga wote pia waliokuwamo ndani ya Hazori kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa; hakubakizwa hata mmoja akiwa hai; kisha akauteketeza Hazori kwa moto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha akauteketeza mji wa Hazori kwa moto na kuwaua wakazi wake wote, asimwache hata mtu mmoja. Biblia Habari Njema - BHND Kisha akauteketeza mji wa Hazori kwa moto na kuwaua wakazi wake wote, asimwache hata mtu mmoja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha akauteketeza mji wa Hazori kwa moto na kuwaua wakazi wake wote, asimwache hata mtu mmoja. Neno: Bibilia Takatifu Kila aliyekuwa ndani yake wakamuua kwa upanga. Wakawaangamiza kabisa, wala hawakusaza chochote chenye pumzi, na akauchoma Hazori kwa moto. Neno: Maandiko Matakatifu Kila aliyekuwa ndani yake wakamuua kwa upanga. Wakawaangamiza kabisa, wala hawakusaza chochote chenye pumzi na akauchoma Hazori wenyewe kwa moto. BIBLIA KISWAHILI Nao wakawapiga wote pia waliokuwamo ndani ya Hazori kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa; hakubakizwa hata mmoja akiwa hai; kisha akauteketeza Hazori kwa moto. |
Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu chochote kipumzikacho;
wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;
Basi Yoshua akaipiga nchi hiyo yote, nchi ya vilima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela, na nchi ya materemko, na wafalme wake wote; hakumwacha aliyesalia hata mmoja; lakini akawaharibu kabisa wote waliokuwa hai, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume, wanawake, watoto na wazee, na ng'ombe, kondoo na punda, kwa upanga.
Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya BWANA.