Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.
Yoshua 10:9 - Swahili Revised Union Version Basi Yoshua akawatokea ghafla; kwani alikwea kutoka Gilgali kwenda usiku kucha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kutembea kutoka Gilgali usiku kucha, Yoshua akawatokea ghafla. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kutembea kutoka Gilgali usiku kucha, Yoshua akawatokea ghafla. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kutembea kutoka Gilgali usiku kucha, Yoshua akawatokea ghafla. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya Yoshua kutembea usiku kucha kutoka Gilgali, akawashambulia ghafula. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya Yoshua kutembea usiku kucha kutoka Gilgali, akawashambulia ghafula. BIBLIA KISWAHILI Basi Yoshua akawatokea ghafla; kwani alikwea kutoka Gilgali kwenda usiku kucha. |
Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
BWANA naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kukwelea kwenda Beth-horoni, na kuwapiga hadi kufikia Azeka, tena hadi kufikia Makeda.
BWANA akamwambia Yoshua, Usiwaogope watu hao; kwa kuwa mimi nimekwisha kuwatia mikononi mwako; hapana mtu awaye yote miongoni mwao atakayesimama mbele yako.
Basi Yoshua akaenda, na watu wote wa vita pamoja naye, ili kupigana nao hapo penye maji ya Meromu ghafla; wakawashambulia.