Naye akawatoa watu waliokuwamo, akawaweka kwenye kazi ya misumeno, na sululu za chuma, na mashoka ya chuma, akawafanyiza kazi tanurini mwa matofali; ndivyo alivyoifanya miji yote ya wana wa Amoni. Kisha Daudi akarudi na watu wote Yerusalemu.
Yoshua 10:15 - Swahili Revised Union Version Basi Yoshua akarudi, na Israeli wote wakarudi pamoja naye, mpaka kambini hapo Gilgali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Yoshua akarudi kambini huko Gilgali pamoja na Waisraeli wote. Biblia Habari Njema - BHND Kisha Yoshua akarudi kambini huko Gilgali pamoja na Waisraeli wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Yoshua akarudi kambini huko Gilgali pamoja na Waisraeli wote. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Yoshua akarudi kambini huko Gilgali pamoja na Israeli yote. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Yoshua akarudi kambini huko Gilgali pamoja na Israeli yote. BIBLIA KISWAHILI Basi Yoshua akarudi, na Israeli wote wakarudi pamoja naye, mpaka kambini hapo Gilgali. |
Naye akawatoa watu waliokuwamo, akawaweka kwenye kazi ya misumeno, na sululu za chuma, na mashoka ya chuma, akawafanyiza kazi tanurini mwa matofali; ndivyo alivyoifanya miji yote ya wana wa Amoni. Kisha Daudi akarudi na watu wote Yerusalemu.
Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizofuata baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.
Ndipo watu wa Gibeoni wakatuma wajumbe kwenda kwa Yoshua huko Gilgali kambini, wakamwambia, Usiulegeze mkono wako hata ukatuacha sisi watumishi wako; njoo kwetu upesi, utuokoe, na kutusaidia; kwa sababu wafalme wote wa Waamori wakaao katika nchi ya vilima wamekutana pamoja juu yetu.