Watu wote wa Israeli wakakutana mbele ya mfalme Sulemani wakati wa sikukuu, katika mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba.
Yohana 7:2 - Swahili Revised Union Version Na sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya vibanda, ilikuwa karibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikukuu ya Wayahudi ya vibanda ilikuwa imekaribia. Biblia Habari Njema - BHND Sikukuu ya Wayahudi ya vibanda ilikuwa imekaribia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikukuu ya Wayahudi ya vibanda ilikuwa imekaribia. Neno: Bibilia Takatifu Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. Neno: Maandiko Matakatifu Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. BIBLIA KISWAHILI Na sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya vibanda, ilikuwa karibu. |
Watu wote wa Israeli wakakutana mbele ya mfalme Sulemani wakati wa sikukuu, katika mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba.
Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za BWANA, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne.
Wakaishika sikukuu ya vibanda, kama ilivyoandikwa, wakatoa sadaka za kuteketezwa za kila siku kwa hesabu yake, kama ilivyoagizwa, kama ilivyopasa kila siku;