Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.
Yohana 6:6 - Swahili Revised Union Version Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema (Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijua mwenyewe atakalofanya.) Biblia Habari Njema - BHND (Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijua mwenyewe atakalofanya.) Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza (Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijua mwenyewe atakalofanya.) Neno: Bibilia Takatifu Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya. Neno: Maandiko Matakatifu Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya. BIBLIA KISWAHILI Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. |
Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.
Lakini kuhusu wajumbe wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuuliza ajabu iliyofanywa katika nchi, Mungu akamwacha, ili amjaribu, ili kwamba ayajue yote yaliyokuwamo moyoni mwake.
Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.
wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba.
aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.
Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.
Ninayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wanaojiita mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;