Yohana 4:40 - Swahili Revised Union Version Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili. Biblia Habari Njema - BHND Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili. BIBLIA KISWAHILI Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. |
Kitambo kidogo tu nilipoachana nao, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa.
Wewe uliye tumaini la Israeli, wewe uliye Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini wewe umekuwa kama mtu akaaye katika nchi, kama mgeni, na kama mtu mwenye kusafiri, ageukaye upande ili kukaa usiku mmoja tu?
Naye alikuwa na dada yake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.
Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.
Na mtu yule aliyetokwa na pepo alimwomba ruhusa afuatane naye; lakini yeye alimwaga akisema,
Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.
Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatusihi sana.
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.