Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawana nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.
Yohana 3:30 - Swahili Revised Union Version Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni lazima yeye azidi kuwa maarufu, na mimi nipungue.” Biblia Habari Njema - BHND Ni lazima yeye azidi kuwa maarufu, na mimi nipungue.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni lazima yeye azidi kuwa maarufu, na mimi nipungue.” Neno: Bibilia Takatifu Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kupungua. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.” BIBLIA KISWAHILI Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua. |
Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawana nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.
Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.
Yeye ajaye kutoka juu, huyo yuko juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yuko juu ya yote.
Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.
Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.