Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijia katika hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.
Yohana 3:28 - Swahili Revised Union Version Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nilisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nanyi wenyewe mwaweza kushuhudia kuwa nilisema: ‘Mimi siye Kristo, lakini nimetumwa ili nimtangulie!’ Biblia Habari Njema - BHND Nanyi wenyewe mwaweza kushuhudia kuwa nilisema: ‘Mimi siye Kristo, lakini nimetumwa ili nimtangulie!’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nanyi wenyewe mwaweza kushuhudia kuwa nilisema: ‘Mimi siye Kristo, lakini nimetumwa ili nimtangulie!’ Neno: Bibilia Takatifu Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Al-Masihi, ila nimetumwa nimtangulie.’ Neno: Maandiko Matakatifu Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Al-Masihi, ila nimetumwa nimtangulie.’ BIBLIA KISWAHILI Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nilisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. |
Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijia katika hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.
Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye Juu, Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake;
Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?