Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Yohana 2:21 - Swahili Revised Union Version Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya hekalu ambalo ni mwili wake. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya hekalu ambalo ni mwili wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya hekalu ambalo ni mwili wake. Neno: Bibilia Takatifu Lakini yeye Hekalu alilozungumzia ni mwili wake. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini yeye Hekalu alilozungumzia ni mwili wake. BIBLIA KISWAHILI Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. |
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.