Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Yohana 2:20 - Swahili Revised Union Version Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arubaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo Wayahudi wakasema, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arubaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?” Biblia Habari Njema - BHND Hapo Wayahudi wakasema, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arubaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo Wayahudi wakasema, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arubaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?” Neno: Bibilia Takatifu Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe wasema utalijenga kwa siku tatu?” Neno: Maandiko Matakatifu Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe wasema utalijenga kwa siku tatu?” BIBLIA KISWAHILI Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? |
Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Ndipo yule Sheshbaza alipokuja, akaupiga msingi wa nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na tangu wakati ule hadi leo imekuwa ikijengwa, wala bado haijamalizika.
Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonesha majengo ya hekalu.
Na watu kadhaa walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema,
Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?