Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?
Yohana 18:34 - Swahili Revised Union Version Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamjibu, “Je, hayo ni maneno yako au wengine wamekuambia habari zangu?” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamjibu, “Je, hayo ni maneno yako au wengine wamekuambia habari zangu?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamjibu, “Je, hayo ni maneno yako au wengine wamekuambia habari zangu?” Neno: Bibilia Takatifu Isa akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe, au uliambiwa na watu kunihusu?” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe, au uliambiwa na watu kunihusu mimi?” BIBLIA KISWAHILI Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? |
Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?
Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetoka wapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lolote.