Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kulia wa Mungu.
Yohana 16:16 - Swahili Revised Union Version Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!” Biblia Habari Njema - BHND “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!” Neno: Bibilia Takatifu Isa akaendelea kusema, “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.” Neno: Maandiko Matakatifu “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.” BIBLIA KISWAHILI Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona. |
Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kulia wa Mungu.
Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Nendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.
Yesu, huku akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.
Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Nilitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba.
Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenituma, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwenda wapi?
Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.
Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenituma.
wale aliojidhihirisha kwao kuwa yu hai, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.