Yohana 16:1 - Swahili Revised Union Version Maneno hayo nimewaambia, msije mkakwazwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu. Biblia Habari Njema - BHND “Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu. Neno: Bibilia Takatifu “Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. Neno: Maandiko Matakatifu “Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. BIBLIA KISWAHILI Maneno hayo nimewaambia, msije mkakwazwa. |
lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa.
Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe.
Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi niliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nilikuwapo pamoja nanyi.
Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lolote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.
mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo;
Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.