Yohana 12:45 - Swahili Revised Union Version Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenituma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma. Biblia Habari Njema - BHND Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote anionaye mimi amemwona yeye aliyenituma. Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma. BIBLIA KISWAHILI Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenituma. |
Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.
Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu;
Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.