Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yohana 10:32 - Swahili Revised Union Version

Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

lakini Isa akawaambia, “Nimewaonesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni kwa ipi kati ya hiyo miujiza mnataka kunipiga mawe?”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

lakini Isa akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yohana 10:32
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa.


Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Pamoja na haya Yeremia akamwambia mfalme Sedekia, Nimefanya kosa gani juu yako, au juu ya watumishi wako, au juu ya watu hawa, hata mkanitia gerezani?


vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.


Yesu akawajibu, Niliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia.


Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.


Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.


Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini;


Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkuu kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma.


habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.


Enyi wanaume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.